Shehe WaGanjoni atumiwa kama Kibaraka Na Jubilee

Date:

Na Osugo Moseti,

Tudor,Mombasa: Kiongozi wa kidini daima ni nguzo ya umoja na mshikamano. Kiongozi wa kidini hapaswi kuwa mnafiki. Leo viongozi wetu wanapigania umaarufu ili kupata maslahi. Mbona ni kazungumza haya? Nalenga Sheikh anayetekeleza ibada katika msikiti mmoja maeneo ya Ganjoni , bwana anayesaliti waumini wa dini kwa kujenga uhasama dhidi ya Mohammed Ali almaarufu Jicho Pevu.

Huyu sheikh Shehena ameanzisha vita baridi ilimradi Mohammed Ali asipigiwe kura na waakazi wa Nyali bila kutoa sababu ya kimsingi. Je, Mohammed Ali ni adui yako? Kwa upekuzi uliofanywa umeweka paruwanja kwamba ni Sheikh Njaa aliyelipwa na watu fulani mashuhuri ndani ya serikali ya Jubilee kueneza porojo na fitina.

Mbona mtu huyo asimlipe kupiga vita ushoga, mauaji ya kiholela, dhulma dhidi ya wakenya, ufisadi, wizi wa mali ya umma na utovu wa nidhamu uilokithiri Mombasa? Mbona Sheikh huyu apoteze mda kuuza utu wake kwa sababu ya visenti? Wameacha kutoa mafunzo ya Mwenyezi Mungu na baada ya swala sasa nikuwatenga waumini vipembeni na kumchafulia mtu jina ilhali mtu huyu ameishi maisha yakutahadharisha maisha yake kwa maslahi ya Kenya nzima.

Malipo ya mtu huyu si majungu na magugu kwa jina la maslahi. Je, hawa ndio viongozi wanaotegemewa kujenga mustakabali wa maeneo yetu? Kama ni Kiongozi anayeshikilia ukweli wa uovu wa Mohammed Ali Mbona asiyasema aliyonayo peupe wazi wazi badala ya kufuata senti za kipumbavu kutoka kwa matajiri na majasusi wanaoogopa Mohammed Ali kuwa Mbunge wa Nyali kwa maovu waliowafanyia watu wa Nyali na wapwani kwa jumla?

Aya za mtu Mnafiki kwake si tatu pekee kuna mpya ya nne ya akionekana apewa hela. Mkumbusheni dini si ya Mamake wala Babaake. Mwambie Nyali si ya Matajiri wake. Na kama ni Mohammed Ali ni watu wanyali watakao amua wala si yeye kibaraka mbakaji dini. Mohammed Ali inshaallah hata mtumie majasusi dhidi yake atashinda kwa uwezo wake Mungu.

Wakenya wanampenda na nguvu za wakenya na wana-Nyali zitampa uwezo wa kuwatetea na kukomboa mali zao zote za wizi zilizo chini ya himaya ya wabakaji wa demokrasia. Ewe Sheikh mnafiki wa Ganjoni hizo baraza zenu za shilingi mbili hazitafua dafu. Hila, ghilba na njama dhidi ya Mohammed Ali zitashindwa na nguvu za wakenya wapenda amani.

Wakristo kwa Waisilamu tutaungana kumchangua mtoto wetu mwana-demokrasia na mtetezi wa wanyonge Mohammed Ali kutokana na rekodi yake safi. 2017 mpaka kieleweke Nyali na Kenya nzima kwa jumla. 2017 ni RAILA ODINGA RAIS NA MOHAMMED ALI MBUNGE WA NYALI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here


Share post:

Subscribe

spot_imgspot_img

Popular

More like this
Related

DR BEN CHUMO ACCUSED OF CHILD ABDUCTION AND INTIMIDATION AS FATHER KEV ODUOR DEMANDS ANSWERS

A bitter custody battle has exploded into the public...

DPP Version: Obado Orchestrated Calculated Plot to Murder Sharon Otieno, Court Urged to Convict

The Office of the Director of Public Prosecutions has...

Kisumu Public Trustee Office on the Spot Over Alleged Embezzlement of Orphans’ Trust Fund

Serious questions are emerging over the management of trust...